Johari RotanaRRRRR
BOOK NOW
ACCOMMODATION 
CLUB ROTANA  
VYUMBA VYA KUPANGA

Sasa Imefunguliwa

Haijalishi unasafiri umbali gani haupaswi kulazimika kuacha eneo lako la amani na faraja. Ndio maana Johari Rotana inakupa huduma ya vyumba vya kupanga vya kifahari ambavyo vinachanganya faraja ya kukaa nyumbani na urahisi wa kuishi kwenye hoteli. Vyumba hivi ni vizuri haswa kwaajili ya wakaaji wa muda mrefu na katika safari za kifamilia. Kila chumba kimekamilika na vifaa vyote vya jikoni na huduma ya msaidizi atakaehakikisha kila mahitaji yako yanapatikana.

Nyenzo:

  • Uunganisho wa mfumo wa Fibre Optic
  • Mashine ya kufua nguo
  • Matumizi ya bure ya eneo la mazoezi, ulingo wa ndondi na bwawa la kuogelea
  • Bei ya chini ya marekebisho na huduma za ndani (ikiwemo maji na umeme)
  • Huduma ya kukufikishia mahitaji ya ndani
  • Urahisi wa kubadilisha mpangilio wa chumba (vyumba venye fanicha na visivyo)
SEA VIEW/ CITY VIEW STUDIO ROOM
VIEW PHOTOS
BOOK NOW

Jisikie uko nyumbani katika chumba cha kisasa chenye utulivu katika Jiji lenye shughuli nyingi la Dar es Salaam cha mita za mraba 43 aina ya Studio Room, ambacho ni kikubwa kimtindo na kinafasi. Kinafaa kwa wageni wa kibiashara au starehe, mahali hapa pa faragha panapoburudisha panajumuisha kitanda aina ya king, jiko, samani na visitawishi vya kisasa na madirisha yanayoanzia sakafuni hadi darini yanayoonyesha mandhari nzuri ya jiji na bandari.

Amenities: Muunganisho wa intaneti, TV yenye chaneli nyingi, simu ya IP ikiwa na ujumbe wa sauti, jiko, baa ndogo, nyenzo za kutengeneza chai/kahawa, sefu ya chumbani, mashine za kufulia, pasi na meza ya kupigia pasi, matumizi ya chumba cha mazoezi ya mwili hotelini, ulingo wa mchezo wa ngumi na bwawa la kuogelea.

SEA VIEW/ CITY VIEW ONE BEDROOM APARTMENT
VIEW PHOTOS
BOOK NOW

Ingia katika sehemu yako ya faragha Jijini ukiwa Johari Rotana. Chumba chetu Kimoja cha Kupanga kikiwa katika mtindo wa kisasa, kinafaa kwa wageni wanaokaa kwa muda mrefu. Chenye ukubwa wa mita za mraba 87, kinajumuisha kitanda aina ya king, samani za kisasa, jiko, meza ya kufanyia kazi na nafasi kubwa zaidi kwa ajili ya kazi au kupumzika baada ya kumaliza siku yenye shughuli nyingi. Furahia starehe ya mandhari nzuri ya anga la jiji na bandari kupitia madirisha yanayoanzia kwenye sakafu hadi darini ambayo yanaingiza nuru ndani ya chumba chako na mwanga wa kifahari wa jua la Dar es Salaam wakati wa mchana na taa za jiji wakati wa usiku.

Amenities: Muunganisho wa intaneti, TV yenye chaneli nyingi, simu ya IP ikiwa na ujumbe wa sauti, baa ndogo, nyenzo za kutengeneza chai/kahawa, jiko lenye kila kitu, mashine ya kufulia, sefu ya chumbani, pasi na meza ya kupigia pasi, matumizi ya eneo la mazoezi ya mwili hotelini, ulingo wa mchezo wa ngumi na bwawa la kuogelea.

SEA VIEW / CITY VIEW TWO BEDROOM APARTMENT
VIEW PHOTOS
BOOK NOW

Terms of Use
Privacy Policy
Cookie Settings
© Copyright 2024 Rotana Hotel Management Corporation PJSC.
CONTACT
LANGUAGE
MENU
This website uses cookies so that we can improve your user experience and measure the performance of our site. If you continue on this website, you will be providing your consent to our use of cookies.
Read our Cookie Statement
ACCEPT