Johari RotanaRRRRR
FROMUSD148PER NIGHT
BOOK NOW
OVERVIEW 
KITUO  
NYENZO ZA HOTELINI  
SPECIAL NEEDS  

Jengo la kisasa kabisa lenye mwonekano wa kipekee lenye nyenzo bora kabisa katikati ya Kitovu cha Biashara ndani ya jiji liliopo pwani ya Bahari ya Hindi, Johari Rotana inawahakikishia wageni ukaaji wa kifahari usiosahaulika. Sehemu ya eneo la mradi wa MNF Square, yenye maduka makubwa ya bidhaa, makampuni makubwa, karibu na bandari na Feri ya Zanzibar, kitovu cha uchumi, maeneo ya biashara, fuko, na vivutio vingine vikubwa; ni chaguo bora kwaajili ya malazi yasiyo na usumbufu na kwa wasafiri wa kibiashara na starehe, vilevile kwa familia zinazotembelea jiji hili lililochangamka. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere upo umbali wa dakika 30 tu kutoka hotelini na Reli Kuu ipo umbali wa dakika kadhaa.

Imejengwa ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wa kisasa, hoteli hii ya nyota 5 ina vyumba na suite za starehe 193 na vyumba vya kupanga 60 vyenye huduma zote, vikiwa na samani za kisasa, teknolojia na burudani za chumbani za kisasa, na nafasi kubwa zaidi ya kupumzika au kufanya kazi wakati wa ukaaji wako. Iwe una ziara fupi ya kwenda Dar es Salaam au unapanga kukaa kwa muda mrefu jijini hapo, Johari Rotana inatoa aina kadhaa za vyumba ili kukidhi matakwa yako.

Ikiwa ni kula chakula kwa namna tofauti, chagua kutoka kwenye maeneo mazuri matatu au Cigar Lounge, kuanzia mgahawa wa siku nzima wa Zafarani wenye bufee kubwa la vyakula vya Kimediterania, Kihindi, Kiarabu na Kiswahili, hadi Kibo Lobby Lounge kwa ajili ya kahawa na vinywaji, na baa iliyochangamka ya Hamilton’s Gastropub ambapo unaweza kujichanganya, kustarehe na kuvutiwa na vyakula murua vya Kiingereza na Kimarekani. Cigar Lounge inakupa hali ya kifahari na ya kipekee kwa wapenda Cigar katika mandhari ya utulivu na hali ya juu.

Kwa muafaka wa 'kujiweka vizuri', Bodylines Fitness na Wellness Club ni sehemu sahihi ya kupumzika na kuongeza nguvu, ikiwa ni sehemu ya kufanyia mazoezi yenye vifaa vyote, bwawa la kuogelea la nje, ulingo wa mchezo wa ngumi, sauna, vyumba vya mvuke na tiba ya kukanda mwili huku wageni watoto wanaweza kufurahia kwenye klabu ya watoto. Ikiwa unapanga kuwa na mkutano, tukio au hafla maalumu, ikiwa ni pamoja na harusi, ukumbi wetu maalumu wa mita za mraba 2,000 ambao ni ukumbi wa hoteli mkubwa zaidi Dar es Salaam na mkubwa kupita yote Tanzania wenye vyumba sita vya mkutano vyenye vifaa vyote pamoja na zana za sauti na video za kisasa kabisa na mapambo ya kisasa, tunakuhakikisha mikutano ya biashara na ya kijamii yenye mtindo na kijanja.

Johari Rotana
Sokoine Drive
Dar es Salaam
Tanzania
T: +255 659 070 800

F: +255 659 070 899

Sasa Imefunguliwa

Dar es Salaam ni jiji la kibiashara la Tanzania lililochangamka na ndilo Jiji kubwa kuptita yote Tanzania. Lipo katika eneo liliopangwa kimkakati pemebezoni ya pwani ya Bahari ya Hindi, jiji hili, ambalo lilianza kama kijiji kidogo cha wavuvi, limepitia mabadiliko ya kisasa na miaka ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki. Leo bandari yake yenye shughuli nyingi ndiyo bandari kuu Tanzania. Balozi nyingi, vilevile mashirika yasiyo ya kiserikali yapo Dar es Salaam yakiwa yamejiimarisha katika jiji hili lililochangamka, ambalo pia lina migahawa mingi, maduka na majengo ya ofisi.

Masalia ya uwepo wa ukoloni wa Kijerumani bado yanaweza kuonekana katika maeneo na majengo jijini kote. Kuna vivutio maarufu vya utalii kama Makumbusho ya Taifa na Makumbusho ya Vijiji yaliyopo sehemu ya wazi yakionyesha makabila ya Tanzania na historia yao, vile vile Kanisa Kuu la Mt. Yosefu (St. Joseph’s Cathedral), Nyumba ya Utume ya Shirika la White Father, Bustani za Mimea, Ikulu ya zamani na masoko mengi ya kupendeza.

Tanzania inasifika kwa kuwa na mazingira ya asili na mbuga za wanyama za kupendeza na Hifadhi ya Baharini ya Kisiwa cha Bongoyo, kilichopo km 7 kaskazini mwa jiji, kimebarikiwa kwa kuwa na maeneo mazuri ya kuogelea na kupiga mbizi, vilevile fuo za kupendeza, visiwa vilivyojitenga na aina nyingi mbalimbali za viumbe wa baharini. Dar es Salaam pia ni lango kuu la kwenda Zanzibar, mkusanyiko wa visiwa vizuri katika Bahari ya Hindi. Huduma maarufu ya feri ya kwenda Kisiwa cha Zanzibar inapatikana upande wa pili wa barabara kutoka Johari Rotana.

LOCAL INFORMATION
Current Date & Time
Lunedì, 29 Apr 2024 - 00:12 (GMT +3)
Current Weather Conditions
Lunedì, 29 Apr 2024 @ 00:00 EAT
24°C (75°F) Umidità: 76%
Vento: Sud Ovest 3.72
Currency Information
Lunedì, 29 Apr 2024 @ 00:01 EAT
TZS ~ Tanzanian Shilling
1 USD = TZS 2595.09   |   1 EUR = TZS 2776.41
*Above rates are interbank/median. Cash and credit card transactions may be subject to local surcharges.

Sasa Imefunguliwa

Gundua ulimwengu wa fahari na madaha hapa Johari Rotana, wenye machaguo ya malazi ya kisasa kabisa na yenye nafasi kubwa yakiambatana na starehe zisizokuwa na mpinzani, nyenzo za chakula na bisahara zinazokupa starehe kwa uzuri na urahisi.

Nyenzo za hoteli hujumuisha:

  • Vyumba na suite 193 na vyumba vya kupanga 60 vyenye huduma zote
  • Cigar Lounge yenye Cigar za kimataifa
  • Sehemu 3 maridadi za kula chakula, pamoja na huduma ya kula chakula chumbani
  • Intaneti yenye kasi ya juu ya fibre optic
  • Sehemu ya mazoezi ya viungo yenye vifaa vyote
  • Bwawa la kuogelea la nje
  • Sauna, vyumba vya mvuke na huduma ya kukanda mwili
  • Bwalo la hotelini kubwa zaidi nchini (mita za mraba 816)
  • Vyumba 6 vya mikutano vyenye vifaa vyote
  • Nyenzo za kufua nguo
  • Maegesho ya magari
  • Ulinzi wa saa 24
  • Huduma ya Daktari kwa muda wowote
  • Vyumba visivyoruhusu kuvuta sigara
  • Huduma ya kuhudumia watoto
  • Ziara za Jijini zinazoongozwa na waongoza watalii ambao ni wataalamu
  • Kukodi magari ya kifahari, kuchukuliwa uwanja wa ndege kwa kulipa ada

Johari Rotana inajali na kuthamini wateja wetu wenye uhitaji maalamu kwa kuhakikisha wanapata mazingira rafiki kulingana na mahitaja yao.

Huduma zinazopatikana:

  • Maegesho ya gari kwa kutumia Valet
  • Urahisi wa kuingia hotelini na viti vya walemavu
  • Lifti kubwa za kutoshea vizuri viti vya walemavu
  • Vyoo vya mahitaji maalum katika migahawa yote, vyumba vya mikutano, na maeneo mengine yote ya umma
  • Korido pana katika hoteli nzima

Maeneo yanayoweza kufikiwa kirahisi:

  • Kibo Lobby Lounge, Zafarani All Day Dining Restaurant, Hamilton's Gastropub
  • Bwawa la nje la kuogelea
  • Zen Spa
  • Duka la zawadi
  • Vyumba vya mikutano na ukumbi wa Almasi




Terms of Use
Privacy Policy
Cookie Settings
© Copyright 2024 Rotana Hotel Management Corporation PJSC.
CONTACT
LANGUAGE
MENU
This website uses cookies so that we can improve your user experience and measure the performance of our site. If you continue on this website, you will be providing your consent to our use of cookies.
Read our Cookie Statement
ACCEPT